Mkuu wa mkoa wa lindi mhe. Zainabu telack amezindua kampeni ya kimkoa ya kufufua mashamba pori kwenye kijiji cha Narungombe wilaya ya ruangwa mkoani humo.
Mhe. Telack amewataka wakulima kufufua mashamba waliyoyatelekeza ili kuchochea uchumi wa mkoa huo na nchi kwa ujumla kupitia zao la Korosho ambalo mkoa huo unashika nafasi ya pili kwa uzalishaji wake.
Mhe.Telack amesema kuwa kampeni hiyo itawahusisha wakulima wa korosho na wataalamu wa kilimo kwa ngazi zote ili kuhakikisha mkoa huo unaongeza thamani na tija ya kilimo cha zao hilo kuanzia shambani.
Mkoa wa lindi unakadiriwa kua na jumla ya mikorosho 12,821,374 inayohudumiwa huku halmashauri ya Nachingwea ikiwa na mikorosho 5,415,197, Liwale mikorosho 3,365,839, Ruangwa 1,133,333 na Manispaa ya lindi ikiwa na mikorosho 224,000.
Aidha mbali na takwimu hizo mikorosho 900,282 inakadiriwa kuachwa porini katika halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa huku mikorosho isiyohudumiwa ikiwa ni 443,40.
Mhe. Telack amewataka vijana kusaidia kuendeleza mashamba pori hayo badala ya kuwaachia wazazi ambao wamekuwa wakishindwa kuyaendeleza kutokana na umri walionao.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa