Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amewataka wakulima kujiwekea uhakika na utaratibu wa kupata huduma ya Afya iliyobora.
Amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Ruangwa alipofanya mkutano na Viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) katika ukumbi wa Rutesco mjini Ruangwa leo Desemba 20 2018.
Alitoa Rai ya kuwataka viongozi hao wajiunge na bima ya afya ambayo ni Shirika Afya na kuwaunganisha na familia zao inayopatikana kwa elf 76,800
Aliendelea kuwasisitiza kwa kuwatajia Faida na ubora wa bima hiyo ya afya ambayo mtu anapaswa kujiunga kwa elf 76,800 na mtu huyo atapata huduma ya afya sehemu yoyote ndani ya Tanzania.
"Hii inaitwa jipimie Ainaaina tofauti na vifurushi vya simu na ndiyo maan Mwanzo tulikuwa na CHF kwa elf 15,000, tukaja CHF iliyoboreshwa elf 30,000 na sasa tuna shirika Afya ya elf 76,800 ambayo mtu anatapata huduma kokote Tanzania na kwenye maduka ya dawa yote yaliyoungwanishwa na mfuko wa Bima ya Afya" amesema Waziri.
Mheshimiwa Waziri aliwataka viongozi wa vyama vya msingi kuwa mabalozi wazuri kwa kuwahamasisha wakulima wao kujiunga na bima ya shirika Afya.
" Najua wananchi wetu watasema hiyo bima ni ghali nyie ndiyo muwe mabalozi wa kuwaelimisha juu ya faida ya bima hiyo kwasababu mmepata bahati ya kupata elimu ya bima hiyo na ukitegemea wananchi wa huku wanategemea hela za msimu jitahidi kuwaelimisha kipindi hiki wanachopokea hela za korosho ili wajiunganishe na bima hiyo" amesema Waziri Ummy
Pia waziri wa Afya amesema mtu akijiunga na bima hiyo ndani ya wiki atapata kadi yake na ndani ya siku 21 ataanza matumizi ya kadi hiyo sehemu yoyote atakayoenda iwe hospitali za serikali, hospitali binafsi na maduka ya dawa yaliounganishwa na mfuko wa bima ya Afya (NHIF).
Naye kiongozi wa Chama cha msingi Ali chikawe aliipongeza serikali kwa kuwaletea Bima hiyo na kuahidi kuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao kwani Bima hiyo inarahisisha sana upatikanaji wa huduma za afya hata zile zenye gharama kubwa.
Aidha aliomba serikali kutowaachia jambo hili wao tu la kuhamasisha wananchi aliomba wananchi wapewe elimu ya bima ya shirika Afya ili kwao iwe rahisi kuendelea kuhamasisha na kutilia msisitizo.
Shirika Afya ni bima ambayo mwananchi anajiunga kwa elf 76,800 kwa mtu mmoja ambaye ni mtu mzima na kwa mtoto elf 50,400 bima hii inamuwezesha mwananchi kupata huduma ya afya ndani ya Tanzania hospitali za serikali, hospitali binafsi na maduka ya dawa yote yaliyoungwanishwa na mfuko wa Bima ya Afya( NHIF).
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa