Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa ametumia mwanya wa wananchi kuchelewa mkutanoni ama kudharau mkutano wa hadhara kwa kuwatoza 5000 kwa kila mwananchi aliyekumbwa na kadhia hiyo na kuelekeza fedha hizo zipelekwe na kusaidia ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chilangalile
Zoezi hilo limefanyika Oktoba 11 mwaka huu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji vya Chilangalile, Makanjiro, Mbangara, Chikonole na Chikoko katika kata ya Makanjiro Wilayani Ruangwa.
" Haiwezekani Mkuu wa Wilaya afike mkutanoni halafu wananchi anaowahudumia wakae majumbani ama kutohudhuria mkutano, hivyo basi ili kukomesha hali hii nakuagiza Mtendaji wa kijiji simamia zoezi la ukusanyaji fedha hizo na itumike kama nilivyoelekeza" Ameongeza Mgandilwa
Mgandilwa amesema kuwa wananchi hawawezi kupata taarifa za maendeleo ya maeneo yao ama kujua taarifa za mapato na matumizi ya serikali ya kijiji kwa kukaa majumbani na kwani wanakosa haki ya kujua kila kinachojiri katika vijiji vyao.
Aidha amekemea vikali tabia hiyo na kusema kuwa isijirudie tena kwani si tabia nzuri na amewataka wananchi hao kuwa na tamaduni za kuhudhuria mikutano ya vijiji kwa wakati uliopangwa.
Mgandilwa amewasisitiza watendaji kutobadili matumizi ya pesa hizo kwa kulipana posho na kwamba kila mwananchi aliyetoa fedha hizo apatiwe risiti na kwamba yoyote atakayebainika kuhujumu fedha ya wananchi atamshughulikia.
Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya huyo amewataka wananchi ambao nyumba zao zimewekwa alama ya X kuanza kuzibomoa na kutii sheria bila shuruti ili kupisha ujenzi wa barabara ambazo ni chanzo kikubwa cha maendeleo.
"Kufuata sheria na taratibu ni wajibu wa kila mwananchi hivyo usisubiri kubomolewa msitafute kuitia lawama serikali nawakati taarifa mmepokea mapema " Amesisitiza Mgandilwa
Aidha amewataka wakandarasi wa TARURA wanaojenga na kukarabati barabara kuhakikisha zinakarabatiwa kwa hali ya juu ili kuwa na kiwango kizuri cha kupitika bila shida.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa