Mwenyekiti mteule wa Halmashauri ya Wilaya Ruangwa Mkoani Lindi, Andrea Chikongwe ambae ni Diwani wa Kata ya Nandagala, amewataka Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri hiyo kuhakikisha wanashirikiana katika kuleta maendeleo.
Chikongwe ametoa kauli hiyo alipokua anatoa neno la shukrani mara baada ya kutangazwa kuchaguliwa na madiwani kuwa mwenyekiti wa halamshauri hiyo Katika uzinduzi wa Baraza la Madiwani ,ambapo ameeleza kuwa jukumu la kuleta maendeleo katika Wilaya hiyo ni la kila kiongozi atakapotimiza wajibu wake.
“Tuna kazi kubwa sana ya kuleta maendeleo katika Halmashauri hii nipe ushirikiano tuweze kuwa na taasisi yenye amani, utulivu na maendeleo” Chikongwe
Pia alitoa pongeze Diwani wa Kata ya Namichinga Mikidadi Mbute kwa kuteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa