Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi David Silinde amekipongeza Kikundi cha Suti Ruangwa kwa kurudisha mkopo wote waliokopa kupitia mfuko wa maendeleo wa wanawake, vijana na walemavu.
Ametoa pongezi hizo tarehe 18/02/2021 alipofanya ziara ya kikazi wilayani Ruangwa na kutembelea Shule ya Sekondari Liuguru , Kikundi cha Suti, shule mpya ya wasichana Ruangwa, Kituo cha Afya Nandagala, Shule mpya ya Sekondari Nandagala, shule ya sekondari Lucas Maria na shule ya sekondari Hawa Mchopa.
Kikundi hicho kinachojishughulisha na shughuli za ushonaji suti Ruangwa mjini kilipata mkopo wa milioni tatu kutoka mfuko wa maendeleo ya wanawake vijana na walemavu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kikiwa na vijana kumi.
Mheshimiwa Silinde aliwataka vijana hao kutafuta eneo kubwa la kufanyia shughuli zao kwani wameshakua kibiashara hivyo wanapaswa wawe na kiwanda cha kufanyia kazi hizo.
Vile vile aliutaka uongozi wa Halmashauri kukipa kipaumbele kikundi hicho katika mikopo mingine kwa sababu ni waaminifu katika kufanya marejesho.
" Serikali inataka kuona vikundi kama hivi vinavyojituma na vyenye uaminifu katika kufanya marejesho kwani wakikopeshwa wakarudisha wanatoa mwanya wa vikundi vingine kukopa tena", amesema Silinde.
Wakati huo huo alisifia ujenzi wa majengo na usimamizi wa shule ya sekondari Lucas Malia na Kituo cha Afya Nandagala kutokana na kuwa na majengo yaliyojengwa kwa kufuata taratibu.
"Kituo cha Afya Nandagala kinapendeza sana majengo yaliyopungua ya famasi na wodi tutaleta hela ili kukamilisha majengo hayo" amesema Silinde.
Mwisho.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa