Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti amewataka wananchi wa Wilaya ya hiyo kujenga nyumba zenye ubora na uimara kwa kufuata taratibu za ujenzi.Pia amewataka mafundi wanaojishughulisha na shughuli za ujenzi wa nyumba kutumia nafasi zao za kiufundi kuwashauri wateja wao viwango vya nyumba imara vinavyoitajika kabla ya kuanza ujenzi.
Ameyasema hayo wakati anaongea wa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha Chinongwe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa, mafuriko hayo yametokea usiku wa kuamkia jana baada ya kunyesha mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.
Mh Mkirikiti aliwapa pole waathirika wote waliokubwa na hali ya kuezuliwa nyumba zao na kuharibikiwa na mashamba ya majumbani na kuwataka kutokutaka tama na hali hiyo.Aidha Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi wa mji wa Ruangwa kuchukua tahadhari mapema kwani hali ya mvua iko maeneo yote hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kudhibiti eneo lake.
“Nimetembea katika nyumba zote zilizokubwa na upepo huo wa jana na nikagundua tatizo hatujengi nyumba zenye ubora na uimara kuanzia sasa viongozi wa kijiji waanze kusimamia masuala ya ujenzi wa nyumba zenye kiwango kunachotakiwa”alisema
Naye Afisa Kilimo aliwataka wananchi kukata mikorosho iliyokaribu na nyumba zao kwani inaweza kuleta madhara makubwa ikiendelea kuachwa, kwasababu mikorosho hiyo aijapandwa kufuata vipimo vinayoitajika.
“Shimo la Mkorosho linatakiwa kuwa na futi mbili ila hiyo mikorosho iliyopandwa majumbani mingi imepandwa kiholela basi naomba ambaye mkorosho wake upo karibu na nyumba na umepandwa bila kipimo husika aukate mara moja kuepusha madhara mengine makubwa”alisema
Mafuriko hayo yameharibu nyumba za watu 55, mashamba ya majumbani na majeruhi 1 ambaye kwasasa amelazwa Hospitali ya Ndanda na hali yake anaendelea vizuri kwasasa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa