Mei 1 huadhimishwa kila mwaka kama Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo wafanyakazi kutoka mataifa mbalimbali hukumbushwa umuhimu wao katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Maandamano, mikutano ya hadhara, na hotuba hutumika kusisitiza haki na ustawi wa wafanyakazi.
Historia ya Mei Mosi
Asili ya siku hii inaanzia mwaka 1886 mjini Chicago, Marekani, ambako wafanyakazi walifanya maandamano wakidai kupunguzwa kwa saa za kazi hadi nane kwa siku. Maandamano hayo yaligeuka kuwa vurugu katika tukio lililojulikana kama “Haymarket Affair”, ambapo polisi na waandamanaji walijeruhiwa na kuuawa. Mwaka 1889, mkutano wa kimataifa wa vyama vya wafanyakazi ulitangaza rasmi Mei 1 kuwa siku ya kuadhimisha haki za wafanyakazi.
Faida za kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi
Kuadhimisha Mei Mosi kuna faida mbalimbali, ikiwemo kuelimisha jamii kuhusu haki za wafanyakazi, kuongeza mshikamano miongoni mwao, kutoa fursa ya kudai mazingira bora ya kazi, kuhimiza uzalendo na uwajibikaji kazini, pamoja na kuwahamasisha waajiri kuheshimu sheria za kazi.
Ikumbukwe, Mei Mosi ni ukumbusho wa historia ya mapambano ya wafanyakazi na jukwaa la kuendeleza mazungumzo ya haki, usawa na maendeleo endelevu katika sekta ya ajira.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa