Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa waingia makubaliano ya awali na Kampuni ya Carbon First Tanzania Limited kwa kusaini hati ya makubaliano ya kufanya biashara ya hewa baina ya Kampuni hiyo na Halmashauri.
Makubaliano hayo yamefanyika leo April 17, 2024 katika Kikao cha kusainiwa kwa hati ya makubaliano ya kufanya biashara ya hewa ukaa kati ya Kampuni ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kilichofanyika katika ukumbi wa Ruangwa Pride Hotel.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe amesema Halmashauri imekubali kuingia makubaliano ya awali na Kampuni ya Carbon First Tanzania Limited kwa kuona umuhimu wa biashara ya hewa ukaa katika Halmashauri kwani itasaidia kutunza mazingira kwa kutunza misitu ya vijiji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kupanga mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji, kuunda sheria ndogondogo za usimamizi wa misitu ya vijiji halikadhalika kukuza uchumi wa Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhe. Chikongwe ameendelea kusema kuwa baada ya makubaliano hayo ya awali Kampuni ya Carbon First Tanzania Limited itaendelea kutoa elimu kwa jamii vijijini kuhusu namna ya kutunza misitu ya vijiji itakayosaidia kukuza uchumi wa Halmashauri na uchumi mwananchi mmoja mmoja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya ameihakikishia Kampuni ya Carbon First Tanzania Limited kama Halmashauri wanaenda kusimamia ulinzi wa misitu ya vijiji ili kuhakikisha inasimama imara kiuchumi kupitia biashara ya hewa ukaa na bajeti inaenda kuongezeka kwani itanufaika kwa kupata faida ya 61% wakati huo Kampuni ya Carbon First Tanzania Limited inaenda kupata faida ya 39%.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa