Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa inayoongozwa na Ndugu Frank Fabian Chonya yapata hati safi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali baada ya ufungaji wa bajeti wa mwaka wa fedha 2022/2023.
Taarifa hiyo imetolewa leo April 8, 2024 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya katika Kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkurugenzi.
Aidha Ndugu Chonya ameishukuru Menejimenti ya Utumishi wa Umma ya Halmashauri kwa umakini na utendaji wao wa kazi uliofanikisha kupata hati hiyo halikadhalika aipongeza timu nzima iliyokwenda Mkoa wa Dodoma kuwasilisha bajeti ya Halmashauri.
Katika hatua nyingine, Chonya amewataka Wakuu wa Idara wahakikishe wafanyakazi walio chini yao wawe wanawahi kazini na kuwajibika kikamilifu kwa ustawi wa Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa