Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa inayoongozwa na Ndugu Frank Fabian Chonya yakabidhiwa darasa na vyoo na Elianje Genesis Company Limited ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hassan Ngoma awataka vijana wazawa kuwajibika, kujituma, kupambana na kuwa waadilifu ili kunufaika na uwekezaji wa Elianje Genesis Company Limited (Wachimbaji wa madini wazawa)
Ameyasema hayo leo April 05, 2024 katika kijiji cha Chingumbwa kilichopo Kata ya Mbekenyera Wilaya ya Ruangwa wakati wa makabidhiano ya chumba cha darasa na vyoo shule ya msingi Chingumbwa kati ya Elianje Genesis Company Limited na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Aidha Mhe. Ngoma ameongeza kwa kusema kuwa vijana ni lazima kuwa na utayari wa kujifunza mambo mbalimbali yatakayowawezesha kuajiriwa au kujiajiri ili waweze kunufaika na Kampuni ya Elianje Genesis na kujikwamua kiuchumi.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Andrew Chikongwe atoa rai kwa wananchi kushirikiana bega kwa bega na Kampuni ya Elianje Genesis
" Wao wameamua kujitoa kwetu kwa kuboresha miundombinu mbalimbali na sisi pia tuna jukumu la kujitoa kwao hata ukimuona mtu yeyote ana dalili za kufanya hujuma toeni taarifa kwao kwani wao wamesaidia jamii yetu" Amesema Chikongwe.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa