Jumla ya Kompyuta Mpakato 100 zinatarajia kugawiwa katika Shule tano za Sekondari, kila Shule Kompyuta Mpakato 20 ili kuongeza chachu ya wanafunzi kujifunza kwa vitendo zaidi na kuongeza ubunifu na kupunguza gharama za ufundishaji.
Hayo yamebainishwa na Afisa Tehama Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia David Nyangaka leo katika kikao kilichohusisha Madiwani, Wakuu wa Idara pamoja na Wakuu wa Shule za Sekondari, Maafisa Elimu Kata pamoja na Walimu wa Tehama Wilayani hapa.
Nyangaka amesema kupitia Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mheshimiwa Kassimu Majaliwa ameweza kuifikia Wilaya ya Ruangwa kwani lengo ni kuboresha ICT katika Shule kupitia NG’Os ya Reneal Education Outrich iliyopo marekani.
“Kupitia mradi huu Wilaya 23 zilizofikiwa na mradi, utoro umepungua kwani mafunzo ni ya vitendo pia yameambatana na mfumo wa kujifunza zaidi ikiwa tumeweka past papers toka mwaka 1988-2023, practical za masomo ya sayansi, vitabu vya ziada na kiada pamoja na notes za masomo yote Tanzania.” amesema Nyangaka.
Kwa nyakati tofauti Walimu pamoja na Madiwani wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa kwa kuwazia mbali zaidi Jimbo lake katika maswala ya Elimu ya kidigitali zaidi itakayoleta tija katika Wilaya ya Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa