Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imesaini mkataba na ubalozi wa serikali ya Japan wa mradi wa ujenzi wa Maabara ya sayansi shule ya sekondari Kassim Majaliwa.
Serikali ya Japan imetoa shiling millioni 195 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara ya sayansi pamoja na manunuzi ya samani.
Afisa Elimu sekondari ndg, Ernest Haule ameishukuru serikali ya Japan kwa niaba ya Halmashauri na kuwataka walimu wa shule hiyo kushirikiana na mafundi kuhakikisha ujenzi wa maabara hiyo unajengwa kwa kufuata taratibu zote kiufundi.
"Tutafanya vizur tutaitendea haki fedha tuliyopata ili tujipe nafasi za kupata fedha zingine kwa ajili ya shule nyingine zinazohitaji majengo mapya ya maabara" amesema Haule
Naye Mkuu wa shule ya Kassim Majaliwa Bi, Irene Komba amesema wanashukuru kwa kupata fedha za mradi huo ambazo zitawasaidi kupunguza kufundisha kwa nadharia na kuanza kufundisha kwa vitendo.
"Tukikamilisha mradi huu suala la ufaulu katika shule yetu kwa upande wa sayansi utaongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo sisi walimu tutahakikisha hizo fedha tunazisimamia kama maelekezo yanavyotaka"amesema Irene
(Mwisho)
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa