• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Fedha za miradi zitumike kama ilivyokusudiwa

Posted on: November 22nd, 2021

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo wilaya ya Ruangwa, hivyo ni lazima fedha hizo zitumike kama ilivyokusudiwa.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza kwamba wenyeviti wote wa kamati za ujenzi wa mradi hiyo ikiwemo ya ujenzi wa vituo vya afya pamoja na shule watoke katika vijiji ambavyo miradi husika inatekelezwa ili kurahisisha usimamizi.

Ameyasema hayo Novemba 22, 2021 wakati akikagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kitandi iliyoko Kata ya Likunja wilayani Ruangwa, Lindi akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Lindi.

Waziri Mkuu amewataka watu wote walioko kwenye kamati zinaosimamia miradi hiyo  wawe waadilifu na wahakikishe wanadhibiti vitendo vya wizi katika maeneo yote yanayotekelezwa miradi na ijengwe kwa viwango. “Lazima tuzilinde fedha zilizotolewa na Rais wetu mpendwa.”

Amesema kuwa mpango wa Mheshimiwa Rais  Samia ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma zote za kijamii ikiwemo Afya, maji, umeme, barabara ili kuwarahisishia kutekeleza shughuli zao “maendeleo haya yote ni kutokana na juhudi za mkuu wa nchi, lazima tumuunge mkono”

“Kiongozi wa nchi ametoa fedha, hatuwezi kuvumilia kuona mtu mzembe kwenye miradi ya Serikali, huu ni ujumbe kwa kamati zote zinazosimamia ujenzi wa miradi nchini. Wananchi wanatajaria kuona miradi hii inakamilika, simamieni miradi na iishe tena kwa viwango, Mheshimiwa Rais Samia anatoa fedha kwa ajili ya miradi hii ya wananchi”

Waziri Mkuu amesema kuwa wajumbe wote wa kamati za ujenzi wa miradi nchini washirikishwe kwenye hatua zote za ujenzi ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ujenzi.

Kwa upande wake, Katibu wa Mradi huo Mwalimu Arafa Msuya amesema ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari ya Kitandi ambayo ni ya bweni itakayosajili watoto wa kike na kiume kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita itapunguza adha ya wanafunzi wa maeneo hayo kutembea umbali mrefu hadi shule ya sekondari ya Likunja.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imepokea shilingi bilioni moja kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa EP4R kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo unaojumuisha miundombinu ya majengo 16 ambayo ni jengo la utawala, majengo matano yenye jumla ya vyumba 13 vya madarasa.

Miundombinu mingine ni ujenzi wa mabweni manne yakiwemo mawili ya wanafunzi wa kike na mawili ya wanafunzi wa kiume, ujenzi wa nyumba mbili za walimu ambazo ni kila mmoja inauwezo wa kuishi familia mbili, ujenzi wa bwala la chakula na jiko la nje, matundu 30 ya vyoo na ujenzi wa kichomea taka.

Nao, mafundi wanaojenga mradi huo kupitia mfumo wa force account wameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo kwa kuwa mbali na kusogeza huduma za jamii karibu na wakazi wa wananchi pia inatoa ajira kwa wananchi wengi hususani wanaoishi katika maeneo ya karibu. Wameahidi kuikamilisha kwa wakati na kwa viwango.


 (Mwisho)

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa