Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrea Chikongwe ametoa shukurani kwa Wakulima na wafanyabiashara wa wilaya hiyo kwa kuendelea kuchangia, maendeleo ya wilaya
Amesema hayo katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo 14/09/2021.
"Ukipita katika mitaa na vijiji vyetu utaona majumba mazuri, maduka na nyumba za kulala wageni vitu hivi vimetokana na juhudi za baadhi ya wakulima na wafanyabiashara kiukweli tunatambua sana mchangao wao katika kuendeleza na kubadilisha muonekano wa Ruangwa" amesema Chikongwe.
Vile vile ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupeleka umeme katika vijiji vyote vya wilayani hali inayopelekea kuwa na nyumba bora, nzuri na zenye umeme.
Mhe Chikongwe amesema "Tunamshukuru Mbunge wa Wilaya ya Ruangwa kwa kutuleta miradi mbali mbali katika Wilaya kuanzia sekta ya afya, elimu na maji".
"Tunamiradi mikubwa na mizuri katika wilaya yetu ila yote hii ni *ushawishi, ushirikiano na kazi kubwa anayoifanya* Mheshimiwa Mbunge tunashukuru sana kwa hili".
Vile vile Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa pamoja limepongeza menejimenti ya Wilaya kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato kupitia ghala la linalomilikiwa na Halmashauri.
Uongezekaji huu wa mapato umetokana na kuanzishwa kwa ushirikiano na Wilaya ambazo vijiji vyao vimepakana na Wilaya ya Ruangwa kama vile kilwa liwale na nachingwea, ushirikiano unaowezesha wakulima wa vijiji hivi kupunguza gharama ya usafirishaji wa mazao yao kwa kuyauza kupitia ghala la Ruangwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa