Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe ametoa wito kwa wazazi kuwasomesha watoto kwa manufaa yao na familia zao.
"Wazazi tujitahidi kusomesha watoto wetu kwani ni faida kwetu na ni msaada mkubwa sana kwetu na ulimwengu wa sasa elimu ni muhimu kwasababu teknolojia inakua kila siku hivyo kama mtoto hajapata elimu atapata tabu sana kwa kizazi tulichopo" Amesema Chikongwe.
Ameyasema hayo leo Julai 28, katika Kikao cha kuhamasisha elimu Kata ya Nandagala kilichofanyika katika shule ya Msingi Mkata iliyopo kijiji cha Namahema "A" Kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa.
Aidha, Mhe. Chikongwe amewashukuru wanakikundi cha wasomi wazawa wa Wilaya ya Ruangwa (Ruangwa Graduates Platform) kwa moyo wao wa kujitoa kwa ajili ya wilaya yao na Taifa kwa ujumla.
Kikundi cha wasomi wazawa wa Wilaya ya Ruangwa (Ruangwa Graduates Platform) kimeanzishwa mnamo mwaka 2021 kikiwa na wanakikundi zaidi ya 12 kinachoongozwa na Mwenyekiti Bi. Madina Mkundi kikiwa na lengo la kuhamasisha masuala ya Elimu, Afya na masuala mbalimbali ya kijamii.
Kwa upande wao wanakikundi cha wasomi wazawa wa Wilaya ya Ruangwa wametoa mafunzo mbalimbali na ushuhuda kwa yale yote waliopitia na kuwasihi wazazi na Wanafunzi walioudhuria mkutano huo kutilia mkazo suala la Elimu kwani kwa ulimwengu wa sasa Elimu ni zaidi ya mkombozi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa