Waziri wa Habari na Utamaduni Dkt Harrison Mwakyembe amewataka wananchi wa Lindi kutumia dhana ya utamaduni ili kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo.
Waziri Mwakiembe ameyasema hayo alipokuwa akifungua tamasha la utamaduni la watu wa mkoa wa lindi linalofanyika katika kijiji cha makumbusho jijini Dar es salaam leo 25/10/2018.
Mheshimiwa Mwakyembe alisisitiza wananchi wa lindi kujishughulisha na masuala ya utamaduni kama vile kuhifadhi na kutunza maeneo ya kihistoria yatakayowavutia watalii kutoka maeneo mbalimbali.
“ Kwa kupitia utamaduni mtaweza kujikwamua kiuchumi amueni kufanya utamaduni kuwa ni chanzo cha kuleta maendeleo, pia nawapongeza kwa nia ya dhati kabisa na ninawasaa jamii nyingine kuinga mfano wa wanalindi katika kuenzi utamaduni” amesema Mwakyembe
Pia amesistiza kuwa wizara ya habari na utamaduni itaendelea kuunga mkono wadau wanaoshughulika na kazi ya kulinda na kutunza utamaduni kwani taifa bila utamaduni ni sawa na taifa mfu.
“ suala la kutunza na kuendeleza utamaduni si suala la serikali tu ni wajibu wajibu wa kila mwananchi kufanya hivyo hivyo tusaidiane kuendeleza na kukuza tamaduni zetu” amesema Mwakyembe.
Aidha waziri Mwakyembe amepongeza uongozi wa mkoa wa lindi kwa dhamira njema ya kufanya tamasha hili la utamaduni na kuendeleza michezo pia alitoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya ya Ruangwa kwa kujenga uwanja wa Majaliwa Stadium uliopo Wilayani humo.
Tamasha hili la utamaduni limeshirikisha wananchi wa Mkoa wa Lindi kutoka katika Wilaya zote 6 na limebeba kauli mbiu isemayo Lindi utamaduni wetu, Urithi wetu kwa maendeleo pia litafanyika kwa siku 4 kuanzia 25-28/10/2018 katika kijiji cha Makumbusho.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa