Diwani mteule wa kata ya Ruangwa Mponda Alipa Bakari ameapishwa rasmi na hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Ruangwa Mjini, Ndg. Esaya Kingu katika Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa RUTESCO mjini Ruangwa tarehe 15/08/2019.
Mheshimiwa Mponda amekuwa rasmi mmoja wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kupitia chama Tawala CCM, baada ya kula kiapo mbele ya Wageni waalikwa, Wataalamu na waheshimiwa Madiwa.
Mponda aligombea nafasi ya udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kupata ushindi bila kupigwa, kwasababu vyama pinzani vilipoteza sifa ya kusimamisha wagombea, hali iliyopelekea Mheshimiwa Mponda kutangazwa kuwa Diwani Mteule wa kata ya Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa