Diwani mteule wa kata ya Mnacho Chilemba Norbert Danieli ameapishwa rasmi na hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Ruangwa Mjini, Ndg. Mwijuma Bakari Bwanga katika Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili ya mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika katika ukumbi wa RUTESCO mjini Ruangwa tarehe 26/01/2018.
Mheshimiwa Chilembo amekuwa rasmi mmoja wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kupitia chama Tawala CCM, baada ya kula kiapo mbele ya Wageni waalikwa, Wataalamu na waheshimiwa Madiwa.
Chilembo aligombea nafasi ya udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuibuka mshindi kwa kupata kura 1,824, waliopiga kura ni watu 2,516, kura zilizoharibika ni 55 na Mgombea wa upinzani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndugu Onesmo Kambona alipata kura 637 hali iliyopelekea Mheshimiwa Chilembo kutangazwa kuwa Diwani Mteule wa kata hiyo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa