Wito umetolewa kwa wakulima kuacha kuuza korosho kwa njia ya chomachoma au kangomba na badala yake wakulima hao wametakiwa kusubiri mfumo wa stakabadhi ghalani utakaokuwa na tija kwao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa ambapo amesema kuwa mfumo huo ni rafiki kwa mkulima kwani haumuibii mkulima kama wa chomachoma kwani mwaka jana kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ufuta uliuzwa kwa shilingi 1600 kwa kilo moja wakati msimu huu umeuzwa hadi shilingi 3060 kwa kilo moja
" Serikali ya awamu ya tano inawajali sana imewaletea mfumo huu ambao unamsaidia mkulima ili muwe matajiri sasa nyie mnakimbilia chomachoma wenye umaskini, hivyo basi sitaki kusikia suala LA kangomba wala chomachoma na niseme tu nikikukamata utapata tabu sana ambapo nisipokukamata wakati unanunua nitakukamata wakati unasubiri kulipwa baada ya kupeleka ghalani" Amesisitiza Mgandilwa
Pamoja hayo ni vema tukaonyesha imani yetu kwa taasisi za kibenki kwa kuweka fedha zetu katika mabenki kwani huko ni sehemu salama ya kuhifadhi pesa na ni dhana potofu kuamini kuwa benki itakuibia hivyo epukeni kuwaamini watu msiowajua kywatolea pesa bank na badala yake toeni na kuhifadhi pesa katika simu na sio kuweka pesa kama zilivyo majumbani kuepuka kuibiwa.
Aidha ameutaka uongozi wa kijiji cha Mbangara waliouza mashamba kutumia fedha hizo kwa shughuli za maendeleo na kwamba wanapofanya shughuli ya kuuza mashamba washirikishe ofisi ya ardhi wilaya, na kwa upande wa walionunua mashamba kuwa na risiti halali za malipo huku akisisitiza viongozi hao kuwasomea wanakijiji taarifa za mapato na matumizi kwenye mkutano wa kijiji kabla ya tarege 30 mwezi huu.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa