Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Joseph Mkirikiti amewataka wananchi wa Ruangwa kugeuza mapori yaliyopo Wilayani humo kuwa mashamba.
Amesema hayo wakati wa maonesho wa shamba darasa la zao la alizeti yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala kata ya Nandagala iliyopo Wilayani Ruangwa.
Mheshimiwa Mkirikiti alisema hayo kutokana na eneo kubwa la Ruangwa kuwa ni mapori hali inayoonesha suala la ulimaji halifanyiki kwa kiasi kikubwa kama inavyotakiwa.
"Acheni kulalamika hali ngumu nawakati mnamaeneo makubwa na yakutosha hembu geuzeni hayo maeneo kuwa mashamba ya Alizeti muone kama kuna mtu atalalamika hali ngumu ya maisha” amesema Mkirikiti.
“Katika utawala wangu wa Wilaya hii sitovumilia suala la kukaa vijiweni, vijana mnakaa vijiweni badala ya kuandaa mashamba mkalima alafu mnalalamika hali ngumu nikikuta vijiwe visivyoeleweka navuvunjilia mbali” amesema Mkirikiti.
Amesema Mkuu wa Wilaya nguvu ya wakulima wanayoiweka kwenye zao la Korosho na Ufuta basi ihamishiwe kwenye zao la alizeti kwani zao hilo linasoko kubwa kama ilivyo korosho na ufuta.
Pia aliwaambia wakulima wa Alizeti changamoto walizozitaja safari hii mwakani hazitokuwa changamoto tena kwasababu watakuwa wamepata mauzo ya kutosha yatakayopelekea kutatua changamoto hizo.
“Msikate tamaa msiwe wanyonge siku zote mwanzo ni mgumu ila mwakani mkilima tena alizeti hizi changamoto hazitokuwepo hivyo jitahidini mkivuna muandae tena mashamba na uzuri wa alizeti ni kilimo cha miezi 3 tu”amesema Mkirikiti.
Naye Salum Lipei Mkulima wa zao la alizeti aliwataka wakulima wenzake kulima zao hilo kwa kisasa zaidi ili waweze kupata mavuno mengi yatakayopelekea kupata mafuta kwa wingi.
“Wakulima wenzangu hili zao linasoko la nje na ndani ya nchi hivyo tuzidishe juhudu ya kulima alizeti inatusaidia katika kupata mafuta na kuongeza kipato tujitahidi kuongeza ukubwa wa mashamba”amesema Lipei.
Nao wenye kikundi cha Chiepo ambao wamelima shamba lililofanyiwa maonesho walilishukuru shirika la AGHAKANI kwa kuwa bega kwa bega katik a kuwasaidia mpaka kufika hapo.
Kikundi kilisema AGHAKAN FOUNDATION imewasaidia kuwapatia elimu ya uzalishaji alizeti kwa njia ya kisasa na kuwaunganisha na wadau ambao waliweza kupata huduma za mbegu za kisasa.
Tumeanza kulima alizeti mwaka 2012 tulikuwa tunatumia mbegu za kizamani na hatukuwa na mafunzo ya uzalishaji wa kisasa ila kuanzia 2018 tunashushuru shirika la AGHAKANI limetuwezesha kupata vyote hivyo kwa urahisi.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa