Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe Hashim Mgandilwa amewataka wachimbaji wote wa Madini wasio na leseni wala mkataba kutoka kwa waajiri wenye mgodi kununua Vitambulisho vya Mjasiliamali.
Ameyasema hayo siku ya tarehe 10/06/2019 alipofanya kikao katika Kitongoji cha Namungo kilichowajumuisha wachimbaji wadogowadogo na wachimbaji wenye leseni.
Katika kikao hicho Mheshimiwa Mgandilwa alisema kuwa kila mchimbaji anapaswa kutambulika na Serikali hivyo ni lazima kila kila mmoja wao anunue kitambulisho cha mjasiliamali.
*"Mnahitaji kupata mikopo ya muda mrefu kama mlivyosema, sasa ili kutambulika mnapaswa kununua vitambulisho kusudi taasisi za kifedha ziweze kuwatambua.”*
*“ninatoa wiki mbili mpaka tarehe 26 kila mchimbaji mdogo ahakikishe anafauata utaratibu wa kununua kitambulisho hiko kama anaitaji kufanya kazi katika mgodi huo " alisema.*
Sambamba na hilo Mheshimiwa Mgandilwa wamewataka wachimbaji wote wenye migodi kufanya kazi na wachimbaji wadogowadogo ambao watakuwa na vitambulisho vya mjasiliamali.
Vilevile katika kikao hiko hiko Mkuu wa Wilaya aliiagiza kamati ya ujenzi wa zahanati ya Namungo kuandaa taarifa ya makusanyo na matumizi ya fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ambayo mpaka sasa aijakamilika.
Alisema kwamba ni wajibu kwa kila kamati kusoma mapato na matumizi ya fedha zilizokusanywa, na ifikapo tarehe 26 atakuja kusikiliza taarifa, na kama ikibainika kuna ubadhilifu, wajiandae kurudisha fedha za wananchi.
Jophery Amani ambaye ni mchimbaji mdogo aliiomba serikali kuwasaidia kupata mikopo ya muda mrefu ili iweze kuwasidia kuendeleza kazi zao.
Vilevile aliomba suala la zana za milipuko zinazotumika katika kazi za uchimbaji ziwe zinapatikana karibu kwani sasa wanachukia zana hizo morogoro hali inayopekelekea kuna muda kuchelewa kwa kazi zao.
*MWISHO*
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa