Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa mheshimiwa Hashim Mgandilwa amewataka watumishi ya Wilaya ya Ruangwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea mara moja na kutoa huduma kwa wananchi kama wanavyotakiwa.
Ameyasema hayo leo 07/08/2018, wakati wa kikao chake na watendaji wa kata, Wazee wa dini, Waratibu Kata na Wakuu wa Idara ,kilichofanyika katika ukumbi wa Narungombe mjini Ruangwa.
Mheshimiwa Mgandilwa aliwataka watumishi kuwathamini na kuwahudumia wananchi kwani wao ndiyo wanaowafanya watumishi kuajiliwa na serikali hivyo ni wajibu wao kuwatumikia.
“Hakuna kiongozi anaependa kutumbua na ninaomba tusifike huko kila mmoja afanye kazi kama ambavyo majukumu yake namtaka kwani sitoweza kuvumilia mtumishi anayeshidwa kutimiza wajibu wake kwa makusudi kabisa” amesema Mgandilwa.
Anayeona anashidwa kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano naomba ajiondoe mapema ampishe mtanzania mwingine anaeweza kufanya kazi kwa bidii na wapo watu wa hivyo.
Pia aliwataka wananchi pamoja na watumishi wa Ruangwa kumpa ushirikano wa kutosha ili kuiimarisha Ruangwa kwani yeye kaja kushirikiana na kuwahudumia wanarungwa,
“Siwezi kusimama mwenyewe katika kufanya mambo ya kimaendeleo katika Halmashauri yetu nishikeni mkono na mie nitawashika mkono ili iwe rahisi katika kuwatumikia wananchi na kuiendeleza Ruangwa” amesema Mgandilwa.
Vile vile aliwataka wakuu wa idara na Vitengo kuhakikisha kila idara inabuni chanzo kipya cha mapato kwani makusanyo ya sasa ya mapato ya ndani ni madogo na hayaridhishi.
“Naona dalili ya siye kuhamia Halmashauri ya Nachingwea kutokana na makusanyo haya madogo tunayokusanya kwani halmashauri itakayoshidwa kujiendesha itavujwa na kwa mahusanyo haya tunaweza kuhamia Nachingwea sasa kuepusha haya kila Mkuu wa idara abuni chanzo kipya cha mapato” amesema Mkuu wa Wilaya.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya Twaha Mpembenwe alimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya mpya Mheshimiwa Hashim Mgandilwa aliyeshika nafasi ya Mkuu wa wilaya Joseph Mkirikiti aliyehamishiwa Wilaya ya Hanang.
“Nikuhakikishie kuwa Wanaruangwa watakupa ushirikano wa kutosha karibu sana Ruangwa jisikie kama upo nyumbani sina mashaka na wanaruangwa wenzangu kwa upande wa ushirikiano” amesema Mpembenwe.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa