Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto katika zoezi la chanjo litakalofanywa kuanzia tarehe 15/10- 19/10/2019.
Mhe. Mgandwila amesema hayo leo tarehe 02/10/2019 wakati wa kikao maalumu cha kamati ya Afya ya msingi(PCH) kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Mhe. Mgandilwa amesema zoezi hilo litakuwa na chanjo ya aina mbili chanjo ya surua Rubella na chanjo ya Polio sindano ambayo itatolewa katika maeneo yote ya Ruangwa.
“Zoezi hili litawahusu watoto wote wenye umri wa miezi 9 hadi chini ya miaka 5 kwa chanjo ya surua na chanjo ya polio ya sindano itawahusu watoto wa mwaka mmoja na nusu mpaka miaka tatu na nusu”
Mkuu wa Wilaya aliendelea kusisitiza kuwa chanjo hizo zina lengo la kitaifa la kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambayo ni surua Rubella na Polio ambayo itakuwa na lengo la kuongeza kinga kwa watoto wote hata kama wameishapata huduma za chanjo kwenye vituo vya Kutolea huduma za afya.
Aidha Mhe. Mgandilwa alisema huduma hii inatolewa bure katika maeneo yote hivyo ni wajibu wa kila mzazi kupeleka mtoto katika sehemu husika itakayokuwa inatolewa huduma hiyo.
Pia amewataka watu watakaopewa dhamana ya kutoa huduma hiyo basi kuifanya kwa weledi na kwa uaminifu kama ambavyo wanatakiwa.
Vile vile Mganga Mkuu wa Wilaya dr Mahile njile aliwaomba viongozi katika ngazi za kata na vijiji kuwasaidia kuhamasisha wananchi ili kila mwananchi apate nafasi ya kumpatia mtoto wake chanjo hiyo.
“Naomba viongozi wa siasa na madiwani mtusaidie kufuatilia zoezi la chanjo itakapotolewa kama watoto katika eneo hilo wote wamepata chanjo hiyo maana ni wajibu kila mtoto aliye chini ya umri wa miaka tano kupata kinga hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kushiriana na Wizara ua Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo inategemea kufanya kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo hizo za aina
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa