Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hashim Mgandilwa amewataka wanaruangwa kuwa na utamaduni wa kusaidia timu ya Namungo Fc iliyonamakazi yake Ruangwa mjini.
Amesema timu ya Namungo inaendeshwa kwa misaada ya wananchi ila kumekuwa na kusua sua michango kutoka wakazi wa Ruangwa kiujumla.
Amesema hayo leo Mei 5/2019 wakati wa halfa ya kuipongeza timu ya Namungo Fc ambayo imefuzu katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara iliyofanyika katika kitongoji cha Namungo kilichopo katika kata ya Mbekenyera kijiji cha Chingubwa Wilaya ya Ruangwa.
"tusiwaachie watu wa nje pekee yao kutuchangia tunapaswa tuoneshe mfano na si lazima uchangie kiasi kikubwa hata iwe shilingi 1000 inapokelewa changieni timu yenu kwenye akaunti husika kwani uzalendo kwanza" amesema Mgandilwa
"Niwahakikishie kila mtu wa Ruangwa atacheza kwa wakati ili kufanikisha tunafuzu mashindano hayo na huko hatuendi kushiriki tunaenda kushinda kwenye mashindano hayo" akisisitiza Mkuu wa Wilaya
Pia alisema sasa kuna timu ya Namungo ambayo ipo Wilayani Ruangwa hakuna sababu ya kushangilia timu nyingine uzalendo kwanza tuache timu zetu za zamani tuhamishie mapenzi kwa Namungo na tuendele kwenda kuishaingilia timu yetu kila inapocheza kama tulivyofanya msimu wa ligi iliyopita.
Aidha aliwaasa wachezaji kuwa mpira ni ajira wanakila sababu ya kuhakikisha nidhamu, kujituma na ushirikiano unatawala kati yao.
" Hakuna mafanikio yanayokuja bila kujituma hamuwezi kupanda bila jitihada mpira ni ajira yenu muipende na kuithamini mtafika mbali " amesema Mgandilwa.
Naye Naibu mwenyekiti wa timu Francis Mwingila ametoa shukurani kwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa msaada aliokuwa anautoa kwa timu tangu inaanza mpaka ilipofikia
Vilevile bwana Mwigila aliishukuru ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa ushirikiano walioutoa wa ndani na nje kwa wachezaji wa timu hiyo.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa