Utiaji wa saini kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na Mkandarasi Tendar International constraction company limited watakaotelekeza kandarasi yote ya ujenzi wa Ghala la kisasa la Wilaya katika kata ya Ruangwa Wilaya ya Ruangwa umefanyika leo Januari 21/2019.
Halfa fupi ya kusaini kandarasi hizo imefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ambapo jumla ya majengo nane muhimu yatajengwa ambayo ni jengo la utawala, magala mawili, Kantini, Majengo ya kupimia uzito, Mnara wa kuwekea matanki ya maji.na jengo kuhifadhia vitu vya umeme, ambayo yanatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi nane (08).
Aidha kiasi cha fedha kitakachotumika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi huu mkubwa na muhimu kwa kuongeza mapato ya Halmashauri na huduma ya kuhifadhi mazao kwa wananchi itakuwa inapatikana kwa uhakika na karibu.
Akizungumza katika halfa hiyo ya kutia saini, Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbya ,Amemtaka mkadarasi huyo atekeleza mradi kwa wakati sanjari na kuzingatia viwango vilivyokubalika na atahakikisha wanapata vifaa na malipo yao kwa wakati ili ghala hilo likamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Halmashauri ya Ruangwa.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri Bw Andrea Chezue ametoa rai kwa wataalamu hao wa ujenzi kufanya kazi kwa weledi mkubwa kuacha visingizio vya mara kwa mara vitakavyochelewesha kukamilika kwa mradi.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa