Baraza la Wafanyakazi Wilaya ya Ruangwa limeafiki bajeti iliyopangwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa mwaka wa fedha 2018-2019 ambayo ni kiasi cha Shilingi Bilioni 36.1 baada ya kuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Wakuu wa Idara na Vitengo kufuatia kuwasilishwa kwa bajeti hiyo.
Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya muwasilisha mada Afisa Mipango Thomas Luambano kuwasilisha bajeti hiyo kama ilivyopangwa na Halmashauri kwa Wajumbe wa Baraza hilo la Wafanyakazi, na Wajumbe hao kupata nafasi ya kutoa hoja zao na kupatiwa majibu na Wakuu wa Idara na Vitengo waliohudhuria kikao hicho.
Hayo yalifikiwa muafaka wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi lililoshirikisha Wajumbe mbalimbali kisheria, kikao hiko kilifanyika katika ukumbi Rutesco mjini Ruangwa 24/01/2018 ikiwa ni mchakato unaofanyika kila mwaka
Bajeti ya Halmashauri ya mwaka 2018-2019 imeongezeka kwa asilimia 19.17 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2017-2018 kutokana na ongezeko la mishahara ya watumishi pamoja na uchangiaji wa wananchi katika sekta ya Afya.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa