Baraza la Madiwani katika Halimashauri ya Wilaya ya Ruangwa limeidhinisha na kupitisha Tsh. billion 35,981,454,000 makadirio ya mpango na bajeti ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Bajeti hiyo imeidhinishwa na Madiwani katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halimashauri ya Wilaya ya Ruangwa leo 16 Februari 2024.
Akiwasilisha bajeti hiyo afisa mipango Halimashauri ya Wilaya ya Ruangwa Patson Masamalo amesema utayarishaji wa bajeti hiyo umezingatia vipaumbele vilivyomo kwenye mpango wa miaka mitano wa maendeleo, Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025, Muongozo wa utayarishaji wa bajeti wa mwaka 2024/2025.
Aidha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2020-2025 pia mpango mkakati ya Wilaya na vipaumbele vya kisekta, sheria za nchi, kanuni na miongozo mbalimbali.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa