Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa siku ya tarehe 26/2019 wakati wa kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika mjini Ruangwa katika ukumbi wa Narungombe pub.
Mhe. Mgandilwa amesema ataanza kuwachukulia hatua za kisheria watoto watoro pamoja wa wazazi wao baada ya tarehe 31/03/2019 na hatua hizo zitaanza baada ya kusajiliwa kwa mahakama tembezi( mobile court) ambayo atakuwa anatembelea kila kata kila kijiji ndani ya Wilaya kwani Mahakama hiyo mpaka kufikia tarehe 31 mwezi huu itakuwa ishaanza kazi.
"Wazazi anzeni kutimiza wajibu wenu kwani mahakama hii ikianza Sitokuwa na msamaha, mzazi atapigwa faini ya laki sita akishindwa atapata kifungo cha miezi mitatu na mtoto ataadhibiwa bakora zitakazotolewa na hakimu"
"Na nyie watoto wenye utoro wa rejareja nawapa salamu zangu hili suala nitalimaliza na nitahakikisha kila mwanafunzi anamaliza kidato cha nne nitakomesha utoro na hali ya watoto kuacha shule" alisema Mgandilwa
Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa hatahakikisha watoto walioanza shule mwaka huu na walioanza mwaka jana na mwaka juzi wanamaliza kidato cha nne, hataki kusikia watoto wanaoishia njiani kwenye masomo katika Wilaya yake.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Rashidi Nakumbya amewataka wadau wa elimu kuyafanyia kazi maazimio yote ya kikao kama walivyokubaliana na ametaka mikakati yote iliyopangwa ikatumike, na idara husika iifuatilie ili kubadilisha hali mbaya ya ufaulu katika Wilaya la Ruangwa.
"Hizi aibu ziwe na mwisho na mwaka jana ndiyo mwisho mikakati inayowekwa ifanyiwe kazi na si panga mambo alafu amyatekelezi"
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Andrea Chezue amewataka walimu kujitahidi kutimiza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi na pia ameagiza kuanzia mwezi wa pili Idara ya Elimu kupita katika shule zote zilizopo Wilaya ya Ruangwa ili kufuatilia mikakati ambayo shule imejiwekea kubadili hali ya ufaulu.
"Serikali tutatimiza wajibu wetu na nyie timizeni wajibu wenu na shirikianeni na wazazi ili tufanikiwe kupandisha hali ya ufaulu. Mwaka 2019 uwe mwaka wa mwisho kufanya vibaya " alisisitiza Chezue
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa