Asilimia 54% ya kaya wilaya ya Ruangwa yatajwa kuwa zenye vyoo takwimu ambazo zimekua mbaya Sana Hali ambayo inapelekea serikali kutumia rasilimali kubwa Sana ya fedha kutumika katika uagizaji wa madawa ya kuzuia magonjwa ya kuharisha.
Hayo yamebainishwa na mganga mkuu wa wilaya ya Ruangwa Dr.Salivio Wikes katika kikao kilichofanyika Leo wilayani hapa DMO Wikes amesema takwimu hizo ni mbaya mno kwani ni Kwa wenye vyoo na vikihesabiwa vyoo Bora takwimu zinaweza shuka zaidi kupitia hayo amewaomba watendaji kuendelea kampeni kuhamasisha ujenzi wa vyoo katika maeneo Yao
"Mkuu wa mkoa alisema wilaya yetu ni ya mwisho na hataki kuona wilaya yetu inakua ya mwisho katika matumizi ya vyoo akasema hii Hali hataki kuiona katika Sensa,chanjo nimeona katika maeneo yetu vyoo hakuna"
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya nachingwea Hashimu Komba akikaimu DC Ruangwa ameonesha kusikitishwa na Jambo Hilo huku akiwakumbusha watendaji kuwa vyoo Bora si Jambo la kukumbushwa"mmevaa vizuri mmependeza watuwenu wanajisaidia nje VEOs pamoja na WEOs shughulikieni Hilo si la mpaka DC atoe tamko au halimashauri iandike barua kuwaambia"DC Komba
Aidha Mtendaji wa kata ya chienjele Reisia Subiria amesema katika kata yake wameanza kuchukua hatua Kwa mpango Kazi ambao umewekwa na wameanza na kijiji cha chienjele hivyo wanaendelea na vijiji vingine na mwananchi ambae hatekelezi hatua zinachukuliwa. Naye Matokeo Mbung'o ambae ni Mtendaji kata ya narung'ombe amesema narung'ombe ina vijiji viwili narung'ombe na liuguru lakin liuguru imekua ni kijiji Chenye changamoto na Kwa mara kadha wananchi wamekua wakifikishwa kwenye vyombo vya Sheria Kwa watu kuchimba mashimo Tu ya vyoo bila kutengeneza vyoo vya kusitiri
"tuna kampeni ya kuondo nyasi kwenye vyoo tunaendelea nayo katika kata yetu ili kupata vyoo vyenye kusitiri"
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa