Afisa Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu George Mbesigwe leo Mei, 4 amekagua jengo la gorofa la shule ya Msingi Likangara na kuridhika na hatua ya ujenzi iliyofikia jengo hilo.
"Mapungufu yaliyopo ni madogo madogo ambayo yanaweza kurekebishika, na kwa hatua hii ujenzi umeenda vizuri" amesema Afisa Mbesigwe.
Aidha Afisa Elimu Mbesigwe amemtaka Mzabuni wa jengo hilo Ndugu Mhoja Mbulugusu kukamilisha mradi huo vitu vichache vilivyobakia ili jengo hilo lianze kutumika.
Pia, Ndugu Mbesigwe amewataka Wahandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kuja kukagua kikamilifu jengo hilo na kujiridhisha kuwa mapungufu machache yaliyobakia yamerekebishwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa