Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Hashim Mgandilwa ameziagiza Serikali za vijiji kuacha kuingia mikataba na watu kabla ya kuifikisha katika Ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya kupitiwa, kwani kukiuka kufanya hivyo mikataba yote itakayosainiwa itakuwa ni batili.
Mhe. Mgandilwa ametoa agizo hilo siku ya tarehe 12/06/2019 kwenye kikao alichokiitisha na Watendaji wa vijiji , Wenyeviti wa Vijiji na viongozi wa vyama vya Ushirika kilichofanyika ofisi kwake ambapo kabla ya kikao hicho alifanya ziara ya kushitukiza katika Maghala ya kuhifadhia mazao na kukuta baadhi ya magunia ya zao la Ufuta yako nje.
"Kata na Vijiji ambavyo mmeingia mkataba na watu bebeni mikataba hiyo muipeleke kwa Mwanasheria wa Halmashauri aiangalie upya kama ni mikataba halali au la"
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya ameagiza viongozi hao kuanza kuingia mikataba na vyama vya ushirika kabla awajaingia mikataba na watu binafsi au mashirika kama walivyofanya sasa.
Akiongea katika kikao hicho, Mhe Mgandilwa amewaagiza viongozi wa kata na vijiji kuacha kuvitoza vyama vya ushirika fedha za gharama za kupanga kwani vyama hivyo vinapaswa kuchangia na si kupangishwa ghala na amevitaka vyama vya ushirika kulipa madeni wanayodaiwa na serikali za vijiji.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Ndg. Mohammed R. Muhidini amewataka watumishi wa umma kufuata sheria na taratibu katika kata zao na si kujiamulia.
Pia alitoa msitizo kwa viongozi hao wa serikali ya vijiji kupeleka mikataba yote iliyosainiwa katika ofisi za serikali ya kijiji ifike ofisi ya Mkurugenzi uharaka iwezekanavyo ili iangaliwe uhalali wake.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa