• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Elimu Msingi



                                                       Mkuu wa Idara Elimu Msingi, Ndg Selemani Mrope


KAZI ZA IDARA

Idara ya Elimu Msingi ndiyo yenye dhamana na kusimamia na kuratibu shughuli zote zinazohusu elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya  Ruangwa. Shughuli hizo ni kama ifuatavyo:- 

  • Kuratibu shughuli zote zinazohusu taaluma katika Halmashauri
  • Kusimamia utendaji kazi wa walimu na watumishi wa idara ya Elimu na wasio kuwa walimu.
  • Kuratibu takwimu zote za Idara ya Elimu kama vile Miundombinu, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, n.k, idadi ya wanafunzi, walimu na nyinginezo.
  • Kuratibu Maslahi ya walimu kama likizo, madai mbalimbali kama vile uhamisho, mizigo na malimbikizo ya mishahara pamoja na kupanda madaraja.
  • Ulinzi na usimamizi wa mali za Umma zitumikazo katika Uendeshaji wa Elimu msingi kama vile Samani za shule, maeneo ya shule na mali nyingine.
  • Kudhibiti utoro wa walimu na wanafunzi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na Kanuni za Elimu na nchi kwa ujumla

 

HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA IDARA YA ELIMU MSINGI 

Idara ya Elimu Msingi inatoa huduma mbalimbali zinazohusiana na mambo ya Elimu na Taaluma kwa wanafunzi, wananchi na Walimu kwa ujumla. Vilevile Idara hii hutoa huduma kama inavyoelekezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwa kuzingatia miongozo, nyaraka na maelekezo mbalimbali. Baadhi ya Huduma zitolewazo ni kama ifuatavyo:

  • Kushughulikia uhamisho wa wanafunzi na walimu
  • Kushughulikia likizo za walimu na watumishi na wasio walimu wanaohudumia katika Idara ya Elimu msingi
  • Kushughulikia masuala ya kinidhamu na utoro wa walimu na wanafunzi.
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wazazi, wanafunzi na walimu kwa ujumla
  • Maslahi ya walimu kama madaraja n.k
  • Huduma mbalimbali zinazohusiana na taaluma

VITENGO VILIVYOPO IDARA YA ELIMU Msingi

TAALUMA

  • Kusimamia ufundishaji na ufungaji shuleni.
  • Kufanya usajili wa wanafunzi wanaofanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) na upimaji wa kitaifa wa Darasa la nne (SFNA).
  • Kwa kushirikiana na Afisa Elimu Watu Wazima kusimamia vituo na madarasa ya elimu nje ya mfumo rasmi na elimu masafa.
  • Kufanya tathimini ya matokeo ya mitihani yote ya kujipima Wilaya, Mkoa na mitihani ya kitaifa.
  • Kupitia taarifa za ukaguzi wa shule zinazofanywa na Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule na kuyafanyia kazi mapendekezo waliyoishauri Idara ya Elimu Msingi.

ELIMU MAALUM

  • Kutoa ushauri wa kitaaluma kuhusu huduma ya watu wenye ulemavu.
  • Kufuatilia na utoaji wa Elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
  • Kusimamia ukusanyaji na utunzaji wa Takwimu za wanafunzi wenye ulemavu.
  • Kufuatilia uandikishaji wa watoto wenye mahitaji maalum.
  • Kufuatilia upatikanaji wa vifaa saidizi vya wanafunzi na vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

ELIMU WATU WAZIMA

  • Kumshauri Afisa Elimu Msingi kuhusu masuala ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya mfumo rasmi EWW/ENMRA.
  • Kusimamia utekelezaji wa sera ya Elimu watu wazima Elimu nje ya mfumo rasmi EWW/ENMRA.
  • Kubaini mipango ya kuendeleza taaluma ya Elimu Watu Wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi.
  • Kuratibu mashindano ya kitaaluma ya Elimu watu wazima Elimu nje ya mfumo rasmi EWW/ENMRA katika Halmashauri.
  • Kukusanya, kuchanganua na kutayarisha taarifa za utekelezaji wa Elimu watu wazima Elimu nje ya mfumo rasmi EWW/ENMRA wa kutoa taarifa.

ELIMU TAKWIMU NA VIFAA (SLO)

  • Upanuzi na uimarishaji wa Elimu Msingi.
  • Kusimamia na kufuatilia ujenzi wa shule.
  • Ukusanyaji, uhifadhi na utoaji wa takwimu za Elimu Msingi (kuzipokea, kuzichanganua, kuzifafanua na kuziwasilisha zinakotakiwa bila kuchelewa).
  • Mahitaji ya walimu – kufanya makisio ya idadi kwa daraja kufuatana na upungufu na upanuzi.
  • Vifaa vya shule – uagizaji na usambazaji kufuatana na mahitaji ya shule na fungu la fedha.
  • Mtihani – usimamizi, usafirishaji na usalama wake
  • Kusimamia fedha katika Idara matumizi yalingane na mahitaji.
  • Kufanya kazi zingine mtakazopewa na Afisa Elimu Wilaya.

UTAMADUNI NA MICHEZO

  • Kuandaa na kuratibu shughuli za michezo ya wanafunzi wa shule za msingi (UMITASHUMTA) shule za Sekondari (UMISSETA) na watumishi walio chini ya mamlaka ya Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
  • Kuratibu shuhguli za Mwenge wa Uhuru.
  • Kukagua kumbi zinazojishughulisha na upigaji disko pamoja na sherehe mbalimbali (burudani mbalimbali).
  • Kuandaa mabonanza ya michezo kwa wanafunzi na watumishi wa Taasisi mbalimbali za Umma na za watu binafs.
  • Kutoa vibali vya matangazo mbalimbali ya biashara na yasiyo ya kibiashara, mikutano, burudani za aina zote.
  • Kutoa mafunzo ya sanaa za maonesho, ufundi na lugha pamoja na kuandaa matamasha ya utamaduni.
  • Kutoa ushauri kwa Mkuu wa Idara juu ya mashuala ya utamaduni na michazo.

 

MATARAJIO YA IDARA 

Idara inatarajiwa kufanya mambo yafuatayo:

  • Kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya Taifa kama vile Mitihani ya Darasa la Nne na la Saba
  • Kuamsha ari ya utendaji kazi kwa walimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
  • Kujenga uhusiano mzuri baina ya walimu, wanafunzi na Jamii inayozunguka shule (wananchi)
  • Kuhakikisha maslahi ya walimu yanaboreshwa na kupatikana kwa wakati kama vile fedha za likizo, uhamisho, kupanda madaraja kwa walimu, makazi bora ya walimu, upatikanaji wa vifaa vya kusomea na kufundisha kwa wakati.
  • Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa Elimu na kuwapatia watoto elimu bora.
  • Kuendesha vikao vya wadau wa Elimu katika Halmashauri ili kuleta tija katika elimu

Matangazo

  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KWA SHULE ZOTE ZA WILAYA YA RUANGWA 2021 December 17, 2020
  • TANGAZO LA KUUZA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA May 25, 2018
  • Tangazo la ujenzi wa hospitali ya Wilaya wodi ya wazazi January 21, 2019
  • matokeo ya kidato cha nne 2018 January 24, 2019
  • Ona zote

Habari mpya

  • DC awataka watendaji kukamilisha miradi ya elimu

    December 24, 2020
  • Wafugaji acheni ubabe- Mhe Ndaki

    December 22, 2020
  • RC aagiza kumalizwa kwa mgogoro wa aridhi Mbute na Nangurugai

    December 17, 2020
  • DC Afanya ukaguzi wa vyumba vya madarasa mapya

    December 16, 2020
  • Ona zote

Video

RAIS MAGUFULI AZINDUA UJENZI WA FLY OVER UBUNGO
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa